Swali 07: Baadhi ya wafanyakazi wa kike sauti zao zinakuwa zenye kunyanyuliwa pindi wanapoongea na marafiki zao wa kiume na baadhi yao wanapeana mikono na madaktari wa kiume na wengineo. Ni ipi hukumu ya Shari´ah juu ya hilo? Je, tunapata dhambi kwa kunyamaza?

Jibu: Jambo la wajibu kwa madaktari wa kike na wa kiume wazichunge hali za wagonjwa na wasizinyanyue sauti zao mbele yao bali wafanye hivo sehemu zengine.

Kuhusu kupeana mikono haifai kwa mwanaume kupeana mikono na mwanamke isipokuwa akiwa ni katika Mahram zake. Haifai ikiwa kama daktari au mgonjwa huyo wa kike sio katika Mahram zake. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mimi sipeani mikono na wanawake.”

´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Ninaapa kwa Allaah kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwahi kamwe kuugusa mkono wa mwanamke. Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapeana nao bay´ah kwa maneno.”

Haifai kwa mwanamke kupeana mikono na wanaume ambao sio Mahram zake. Asipeane mikono na daktari wa kiume, mudiri, mgonjwa wala wengineo ambao si Mahram zake. Bali awazungumzishe tu kwa maneno mazuri na awatolee salamu. Lakini hata hivyo pasi na kupeana nao mikono na kujiachia wazi. Asitiri kichwa chake, mwili wake na uso wake japo kwa Niqaab. Kwa sababu mwili wote wa mwanamke hautakiwi kuonekana na mwanamke ni fitina. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

وَإِذَا سَأَلْتُمُوهُنَّ مَتَاعًا فَاسْأَلُوهُنَّ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ ۚ ذَٰلِكُمْ أَطْهَرُ لِقُلُوبِكُمْ وَقُلُوبِهِنَّ

“Mnapowauliza [wake zake] haja yoyote, basi waulizeni nyuma ya pazia. Hivyo ni utwaharifu zaidi kwa nyoyo zenu na nyoyo zao.”[1]

وَقُل لِّلْمُؤْمِنَاتِ يَغْضُضْنَ مِنْ أَبْصَارِهِنَّ وَيَحْفَظْنَ فُرُوجَهُنَّ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا ۖ وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَىٰ جُيُوبِهِنَّ ۖ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ آبَائِهِنَّ أَوْ آبَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ أَبْنَائِهِنَّ أَوْ أَبْنَاءِ بُعُولَتِهِنَّ أَوْ إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي أَخَوَاتِهِنَّ أَوْ نِسَائِهِنَّ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُنَّ أَوِ التَّابِعِينَ غَيْرِ أُولِي الْإِرْبَةِ مِنَ الرِّجَالِ أَوِ الطِّفْلِ الَّذِينَ لَمْ يَظْهَرُوا عَلَىٰ عَوْرَاتِ النِّسَاءِ ۖ وَلَا يَضْرِبْنَ بِأَرْجُلِهِنَّ لِيُعْلَمَ مَا يُخْفِينَ مِن زِينَتِهِنَّ

“Na waambie waumini wanawake wainamishe macho yao na wahifadhi tupu zao na wala wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa yale yanayodhihirika; hivyo waangushe khimari zao mpaka vifuani mwao. Na wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa kwa waume zao, baba zao, baba za waume wao, wana wao wa kiume, wana wa kiume wa waume zao, kaka zao, wana wa kiume wa kaka zao, wana wa kiume wa dada zao, wanawake wao [dada zao wa Kiislamu], wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume, watumishi wanaume wasio na matamanio [tena kwa wanawake], au watoto ambao [bado] hawaelewi [kitu kuhusu] yanayohusu uke. Na wala wasipige miguu yao [wanapotembea] yajulikane yale wanayoyaficha katika mapambo yao.” [2]

Kichwa na uso ni miongoni mwa mapambo makubwa. Kadhalika yale mapambo yanayokuwa mikononi au miguuni yote ni fitina kutokana na Aayah mbili zilizotajwa. Kinachokusudiwa ni kwamba yeye wote ni fitina. Hivyo ni lazima ajisitiri na ajiweke mbali na sababu za fitina ambazo moja wapo ni kupeana mikono.

[1] 33:53
[2] 24:31

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Mariydhw, uk. 25-27
  • Imechapishwa: 06/05/2019