21- Abu Daawuud amepokea kupitia kwa Thawbaan, mtumwa wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Nani mwenye kunidhamini kutowaomba watu chochote nimdhamini Pepo?” Thawbaan akasema: “Mimi.” Akasema: “Usimuombe yeyote kitu.”

Ameipokea Ibn Maajah ambaye amezidisha:

“Thawbaan (Radhiya Allaahu ´anh) alipokuwa juu ya mpango wake na anaponyokwa na fimbo yake hamuombi yeyote ampe nayo. Anateremka mwenyewe na kuichukua.”[1]

22- Ibn Abiy-Dunyaa amepokea kupitia kwa Abu Dharr ambaye amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliniita na kunambia: “Utakubali kuniahidi kiapo cha usikivu na utiifu na utapata Pepo kwa hilo?” Nikasema: “Ndio” na nikanyoosha mkono wangu. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akataka kutoka kwangu: “Usiwaombe watu kitu.” Nikasema: “Ndio.” Akasema: “Wala fimbo yako inapokuanguka. Teremka na ujiokotee mwenyewe.”[2]

[1] Abu Daawuud (1639), Ahmad (5/275) na Ibn Maajah (1837). Swahiyh kwa mujibu wa Albaaniy katika ”Swahiyh-ul-Jaamiy´”.

[2] al-Qanaa´ah wat-Twa´ffuf (01).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad al-Qurtwubiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Hirsw biz-Zuhd wal-Qanaa´ah, uk. 27-28
  • Imechapishwa: 18/03/2017