68. al-´Ayyaashiy upotoshaji wake wa kumi wa Aal ´Imraan


al-´Ayyaashiy amesema:

“Abu ´Amr az-Zubayriy ameeleza kuwa Abu ´Abdillaah amesema kuhusiana na maneno ya Allaah (Ta´ala):

وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ ۚوَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

“Wawepo kutoka kwenu watu wanaolingania kheri na kuamrisha mema na unaokataza maovu. Hao ndio waliofaulu.”[1]

“Katika Aayah hii wanakufurishwa waislamu watenda madhambi. Kwa sababu yule asiyeita katika mambo ya kheri, akaamrisha mema na akawakataza waislamu yale ambayo ni maovu sio katika ule Ummah ambao Allaah ameusifia. Nyinyi mnadai kuwa waislamu wote ni katika Ummah wa Muhammad ilihali Aayah hii inausifia Ummah wa Muhammad kwa sura ya kulingania katika kheri na kuamrisha mema na kukataza maovu. Ni vipi yule asiyekuwa na sifa hizi na isitoshe anaenda kinyume na yale ambayo Allaah ameshurutisha juu ya Ummah na kuusifia kwazo atakuwa ni katika wao?”[2]

Msomaji anaona namna ambavyo Baatwiniy huyu anavyoukufurisha Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), na khaswa Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwa maasi. Uhalisia wa mambo ni kuwa Raafidhwah Baatwiniyyah ndio wenye kuamrisha maovu makubwa, kuita kwayo, kukataza mema na ndio wenye kuwapiga vita kwelikweli wale wenye kutenda matendo mema na khaswa khaswa Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] 03:104

[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/195).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 105
  • Imechapishwa: 03/04/2017