Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya nguzo hizi sita ni maneno Yake (Ta´ala):

لَّيْسَ الْبِرَّ أَن تُوَلُّوا وُجُوهَكُمْ قِبَلَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ وَلَـٰكِنَّ الْبِرَّ مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالْكِتَابِ وَالنَّبِيِّينَ

“Si wema pekee kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi. Lakini wema khaswa ni yule mwenye kuamini Allaah na siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii.” (al-Baqarah 02 : 177)

Dalili ya Qadar ni maneno Yake (Ta´ala):

إِنَّا كُلَّ شَيْءٍ خَلَقْنَاهُ بِقَدَرٍ

”Hakika sisi kila kitu Tumekiumba kwa makadirio.” (al-Qamar 54 : 49)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 117
  • Imechapishwa: 02/06/2020