Amelaaniwa mwanamke anayenyanyua sauti japo ni kwa kumtaja Allaah?


Swali 332: Ni kipi ukijuacho kuhusu Hadiyth ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah amlaani mwanamke mwenye kunyanyua sauti yake japokuwa ni kwa kumtaja Allaah”?

Jibu: Hadiyth ambayo haikuthibiti. Mola (´Azza wa Jall) amesema katika kitabu Chake kitukufu:

وَقُلْنَ قَوْلًا مَّعْرُوفًا

“Semeni kauli inayokubalika.” (33:32)

 فَلَا تَخْضَعْنَ بِالْقَوْلِ فَيَطْمَعَ الَّذِي فِي قَلْبِهِ مَرَضٌ

”Msilegeze kauli asije akaingiwa tamaa ambaye moyoni mwake mna maradhi.” (33:32)

Lau mwanamke atasema “Subhnaan Allaah”, “Allaahu Akbar” na akatamja Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) hakuna neno juu yake – Allaah akitaka.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ijaabatu as-Saa-il, uk. 573
  • Imechapishwa: 15/12/2019