Swali 06: Yule ambaye kwenye nguo zake kuna damu iliyobaki aswali nazo au asubiri mpaka pale atakapoletewa nguo safi?

Jibu: Aswali vile hali yake ilivyo. Asiiache swalah mpaka ukatoka wakati wake. Bali atatakiwa kuswali vile hali yake ilivyo ikiwa hakuweza kuziosha au kuzibadilisha kwa nguo zengine zilizosafi kabla ya kutoka kwa wakati. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]

Ni lazima kwa muislamu kuosha ile damu iliyoko au aibadilishe nguo najisi kwa nguo nyingine iliosafi akiweza kufanya hivo. Asipoweza kufanya hivo basi aswali vile hali yake ilivyo na wala si lazima kwake kuirudi kutokana na Aayah tukufu [iliotangulia hapo juu]. Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yale niliyokukatazeni yaacheni na yale niliyokuamrisheni basi mcheni Allaah muwezavyo.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

[1] 64:16

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Mariydhw, uk. 25
  • Imechapishwa: 05/05/2019