57. Kupoteza damu kunaharibu swawm?


Swali 57: Kuna mtu alikanyaga msumari kazini kwake na damu ikaanza kutoka kwenye mguu wake. Je, hili linaharibu swawm?

Jibu: Haliharibu swawm. Kubwa linaloweza kusemwa ni kwamba mwili wa mfungaji unadhoofika ikiwa damu yenye kutoka ni nyingi.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaas-Swiyaam, uk. 74
  • Imechapishwa: 13/06/2017