54. Kutofaa kumuozesha ambaye kishabaleghe bila idhini yake

2 – Kuhusu kumuozesha ambaye kishabaleghe haifai isipokuwa kwa idhini yake. Idhini yake ni kule kunyamaza kwake. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Bikira haozeshwi mpaka atakwe idhini.” Wakasema: “Ee Mtume wa Allaah! Ni vipi inakuwa idhini yake?” Akasema: “Akinyamaza.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Ni lazima kupatikane idhini yake hata kama mwenye kumuozesha ni baba yake kutokana na maoni sahihi zaidi ya wanachuoni.

´Allaamah Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema katika “al-Hadyi an-Nabawiy”:

“Haya ndio maoni ya wanachuoni wengi na madhehebu ya Abu Haniyfah, Ahmad katika moja ya mapokezi kutoka kwake na ndio maoni ambayo tunamwabudu Allaah kwayo na wala hatuamini vyenginevyo. Na ndio maoni yanayoafikiana na hukumu ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na maamrisho na makatazo yake.”[1]

[1] (05/96).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tanbiyhaat, uk. 104
  • Imechapishwa: 19/11/2019