52. al-Qummiy upotoshaji wa kumi na tatu wa al-Baqarah

al-Qummiy amesema pindi alipokuwa akifasiri Aayah:

يُؤْتِي الْحِكْمَةَ مَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُؤْتَ الْحِكْمَةَ فَقَدْ أُوتِيَ خَيْرًا كَثِيرًا ۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ

“Humpa hikmah Amtakaye, na anayepewa hikmah basi kwa hakika amepewa kheri nyingi. Na hawakumbuki [haya] isipokuwa wenye akili.”[1]

“Kheri nyingi ni kuwa na utambuzi juu ya kiongozi wa waumini na maimamu.”[2]

Tafsiri hii ni upumbavu na ni kucheza na maana ya Qur-aan. Ni jambo zuri kuwa na utambuzi juu ya kiongozi wa waumini na familia ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), lakini sio katika nguzo, wajibu wala sharti za Uislamu. Kila sharti ambayo haikutajwa katika Kitabu cha Allaah ni batili.

Kuwa na utambuzi juu ya kiongozi wa waumini na maimamu kwa mujibu wa Raafidhwah hilo linapelekea kuwakufurisha Maswahabah, kuipotosha Qur-aan na upumbavu mwingine unaoharamishwa na kuchukiwa na Allaah. Bali huku ni kumkufuru Allaah, Kitabu Chake na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu utambuzi huu unabomoa Kitabu cha Allaah na kila kilichomo katika ´Aqiydah, matendo, uadilifu na wema.

[1] 02:269

[2] Tafsiyr al-Qummiy. (1/92).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 84
  • Imechapishwa: 03/04/2017