51. al-Qummiy upotoshaji wa kumi na mbili wa al-Baqarah

al-Qummiy amesema alipokuwa akifasiri Aayah:

فَمَن يَكْفُرْ بِالطَّاغُوتِ

“Basi atakayekanusha ukafiri… “[1]

“Ni wale waliopokonya haki ya familia ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa dhuluma.”

فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ

“… kwa hakika atakuwa ameshikilia imara kishikilio madhubuti… “

Bi maana uongozi.

لَا انفِصَامَ لَهَا

“… kisichovunjika.”

Kamba isiyovunjika. Bi maana kiongozi wa waumini na maimamu.”

اللَّـهُ وَلِيُّ الَّذِينَ آمَنُوا

“Allaah ni Mlinzi wa wale walioamini.”[2]

Bi maana wale wenye kufuata familia ya Muhammad (´alayhis-Salaam).

يُخْرِجُهُم مِّنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۖ وَالَّذِينَ كَفَرُوا أَوْلِيَاؤُهُمُ الطَّاغُوتُ يُخْرِجُونَهُم مِّنَ النُّورِ إِلَى الظُّلُمَاتِ

“Anawatoa kutoka katika viza na kuwaingiza katika nuru. Na wale waliokufuru walinzi wao ni ukafiri… “

Bi maana wale madhalimu dhidi ya familia ya Muhammad na wale wenye kuwafuata. Uhalisia wa mambo ni kwamba Aayah iliteremshwa namna hii:

يخرجونهم من النور إلى الظلمات أولئك أصحاب النار هم فيها خالدون و الحمد لله رب العالمين

“Anawatoa kutoka katika nuru na kuwaingiza katika viza. Hao ni watu wa Motoni wao humo ni wenye kudumu – na himdi zote ni za Allaah, Mola wa walimwengu.”[3]

Ukengeushaji huu unatisha na una kuwakufurisha Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio ambao walimuamini Allaah na wakakufuru ukafiri. Allaah ni Mlinzi wao na wao ni marafiki Wake. Allaah aliwatoa katika viza na kuwapeleka katika nuru ya Tawhiyd na ya imani na akawaokoa kutokamana na Moto kwa Qur-aan na Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Maadui wao ni marafiki wa ukafiri katika mayahudi, manaswara, Baatwiniyyah na waabudu makaburi na makuba wanavyoviabudu badala ya Allaah. Wanajikurubisha kwa makaburi haya kwa kuyachinjia na kuyatolea mirundo ya mapesa. Wanayaabudu badala ya Allaah. Wanayaomba uokozi wakati wa shida. Wanaitakidi kuwa maiti wanajua mambo yaliyofichikana na wanaendesha ulimwengu. Wanapenda na kuchukia kwa ajili yao. Hakika wao ndio wako katika viza vya ujinga, shirki na upotevu. Waislamu na familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hawana lolote kuhusiana na wao.

Tazama jinsi huyu zandiki anaongeza katika Aayah hii tukufu sentesi “na himdi zote ni za Allaah, Mola wa walimwengu” na kusema:

“Namna hii ndivyo ilivoteremka.”

Hivi kweli huoni namna wanavyomsemea uongo Allaah na Kitabu Chake? Halafu wanawatuhumu Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allahu ´alayhi wa sallam) kuongeza na kupunguza katika Qur-aan. Lakini Allaah anawachunga na anavunjavunja njama zao na kufichua hila zao na kumzulia kwao uongo na kuwazulia uongo Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambao ndio marafiki, waaminifu Wake na wachaji Allaah.

[1] 02:256

[2] 02:257

[3] Tafsiyr al-Qummiy. (1/84-85).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 83
  • Imechapishwa: 03/04/2017