50. Nasaha za al-Khattwaab al-Makhzuumiy al-Qurashiy kwa mwanae

1 – Ee mwanangu kipenzi! Lazimiana kumcha Allaah na kumtii. Jiepushe na maharamisho Yake kwa kufuata njia Yake na alama za njia ili yarekebike mapungufu yako na uwe mwenye furaha.

2 – Mtii baba yako na tosheka na nasaha zake. Yazingatie hayo kikamilifu.

3 – Nakutahadharisha na porojo na kucheka sana, mizaha na kuwadhihaki ndugu. Kwani hayo yanaondosha heshima na kuleta chuki.

4 – Hakikisha ni mwenye thamani na heshima pasi na kuwa na kiburi wala majivuno.

5 – Mpokee rafiki na adui yako kwa uso wenye maridhawa. Jizuie na kuwadhuru pasi na kuwadhalilisha wala kuwaogopa.

6 – Kuwa mkati na kati katika mambo yako yote. Bora ya mambo ni yale ya kati na kati.

7 – Zungumza machache.

8 – Wasalimie watu.

9 –  Tembea kwa kunyooka na kati na kati.

10 – Usikae kwenye masoko wala usifanye maduka yakawa ndio mahali pa makutano yako.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Hibbaan al-Bustiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Rawdhat-ul-´Uqalaa’ wa Nuzhat-ul-Fudhwalaa’, uk. 198
  • Imechapishwa: 18/08/2021