50. Makundi matatu ndani ya al-Faatihah


Allaah (Ta´ala) ametaja makundi matatu katika Suurah “al-Faatihah”:

1 – Walioneemeshwa.

2 – Walioghadhibikiwa.

3 – Waliopotea.

Kwa hivyo wewe unamwomba Allaah akuongoze njia ya wale walioneemeshwa. Nao ni wale walioneemeshwa kwa elimu na matendo. Sambamba na hilo unamwomba Allaah akulinde na njia ya wale walioghadhibikiwa. Nao ni wale wanaoitambua haki na wasiitendee kazi. Mfano wa mayahudi na watu mfano wao. Aidha akulinde na njia ya wapotofu. Nao ni wale wanaomwabudu Allaah juu ya ujinga na upotofu. Kama mfano wa manaswara na watu mfano wao.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 83
  • Imechapishwa: 21/06/2022