5. Shari´ah ya wanawake kuswali mkusanyiko

[6] Imewekwa katika Shari´ah kwa wanawake kuhudhuria swalah hizi kujengea Hadiyth ya Abu Dharr iliyotangulia. Bali inafaa kuwateulia imamu ambaye atakuwa ni wa kwao peke yao mbali na yule imamu wa wanaume. Imethibiti kuwa ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) pindi alipowakusanya watu juu ya swalah za nyusiku, alimteua Ubayy bin Ka´b kuwa imamu wa wanaume na Sulaymaan bin Abiy Hathmah kuwa wa wanawake. ´Arfajah ath-Thaqafiy amesema:

“´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) alikuwa akiwaamrisha watu kuswali mwezi wa Ramadhaan na akiwateulia wanaume imamu na wanawake imamu na mimi ndiye nilikuwa imamu wa wanawake.”[1]

Naonelea kuwa kitendo hichi ni sahihi ikiwa msikiti ni mpana ili wamoja wasiwashawishe wengine.

[1]  Hiyo na ile iliyo kabla yake amezipokea al-Bayhaqiy (02/494). Ya kwanza ameipokea vilevile ´Abdur-Razzaaq katika “al-Muswannaf” (4/258/8722) na Ibn Naswr ameipokea katika “Qiyaam Ramadhwaan”, uk. 93, na ameitumia kama hoja kwa yale tuliyoyataja punde tu katika ukurasa wa 95.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qiyaam Ramadhwaan, uk. 21-22
  • Imechapishwa: 07/05/2019