5. Mnasemaje juu ya huruma, Kushuka kwenye mbingu ya dunia na kadhalika?

Swali 5: Mnasemaje kuhusu rahmah, kushuka kwenye mbingu ya dunia na mfano wa hayo?

Jibu: Tunaamini na kuthibitisha yale yote ambayo Allaah amejisifu Mwenyewe kwa rahmah, kuridhia, kushuka na kuja. Kadhalika kwa yale yote ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemsifu nayo. Hili linatakiwa kufanywa kwa njia isiyofananishwa na kiumbe yeyote, kwa sababu Hakuna chochote kinachofanana Naye.

Kama jinsi Allaah ana dhati isiyofanana na dhati nyinginezo, kadhalika ana sifa zisizofanana na sifa nyinginezo.

Hili linathibitishwa na yale mapambanuzi makubwa katika Qur-aan na Sunnah ambapo sifa zimethibitishwa na ambapo Allaah amesifiwa nazo. Humo kadhalika amebainisha kutakasika na anaolingana Nao, wenza na washirika.

  • Mhusika: Imaam ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahamm-ul-Muhimmaat, uk. 33
  • Imechapishwa: 25/03/2017