49. Mwenye busara na kuficha siri


1 – Ni wajibu kwa mwenye busara kuficha siri yake ni mamoja kwa mtu ambaye ni mwaminifu au mwengine. Kabla au baadaye zitatokewa na kitu kitachomfanya yeye kufichua siri zake.

2 – al-Madaainiy amesema:

“Ilikuwa inasemwa kwamba ambaye ana subira yenye nguvu kabisa ni yule asiyemfichulia siri yake rafiki yake kwa kuchelea kusije kutokea kitu akaja kuifichua.”

3 – Ambaye anaficha siri yake basi itakamilika mipango yake, atafikia malengo yake na atasalimika kutokamana na kasoro na madhara. Asipofikia yale anayotarajia, basi anaificha siri yake ndani ya chombo na anaificha kutokamana na kila mtu. Akilazimika kuifichua, basi humweleza nayo kwa mtu ambaye anamtakia mema. Kwani siri ni amana na kuifichua ni khiyana. Moyo una chombo chake; vipo vyombo ambavo vinabeba kiasi kikubwa na vyengine havibebi kiasi kikubwa.

4 – Ibn-ul-´Araabiy amesema:

“Ilikuwa inasemwa kwamba mwenye busara ni yule mwenye kujihadhari na rafiki yake.”

5 – Ni kutokuweza mtu akashindwa kuchunga siri. Kwa sababu mtu amemficha adui yake kitu haina maana kwamba atamfichulia nacho rafiki yake. Inatosha uzoefu kuwa mafunzo kwa wale wenye busara. Yule mwenye kusikia siri asiwe mwenye kuivunja wala kuisambaza. Siri imeitwa siri kwa sababu haienezwi. Kwa ajili hiyo ni wajibu kwa mwenye busar kifua chake kiwe kipana juu ya siri yake kuliko kifua cha mwingine na ahakikishe haifichui.

6 – Ushindi hauji isipokuwa kwa maamuzi. Maamumi hayaji isipokuwa kwa kutafakari. Kutafakari hakuji isipokuwa kwa kuchunga siri. Mwenye kuficha siri yake anakuwa na khiyari. Anayewaeleza watu siri zake basi hudharauliwa mbele ya macho yao na siri yake wanakuwa ni wenye kuitangaza. Ambaye hafichi siri yake basi anastahiki majuto. Yule anayestahiki majuto basi huwa na akili pungufu. Yule mwenye kuendelea juu ya hali hiyo basi hurudi ujingani.

7 – Ni wajibu kwa mwenye busara kutambua kwamba mwenye kutaka mashauriano hufichua siri. Kwa hivyo asimtake mashauri isipokuwa yule ambaye ni mwenye busara, mwenye kumtakia mema, mwenye mapenzi na mtu mwenye dini. Kutaka mashauri kutoka kwa mtu aliyesifiwa namna hii kuna baraka.

8 – al-Hasan al-Baswriy amesema:

“Yule anayemuomba mshauri ushauri basi hatojuta.”

9 – Kikosi cha watu kikiomba ushauri na nasaha na mwenye busara yuko kati yao, basi ahakikishe kwamba yeye ndiye wa mwisho kutoa shauri. Kwa sababu kunafanya kuwa na muda mrefu wa kufikiri na kumkinga kutokamana na kukosea. Katika hali hii kuna uwezekano mkubwa wa kuwa mtu wa maamuzi na khatari ndogo ya kukosea. Yule anayeomba ushauri na nasaha basi ahakikishe hamwombi mtu asiyekuwa na uwezo kama ambavo mtu hamwombi msaada chauvivu. Kuomba ushauri ni  mwongozo safi. Yule anayeomba ushauri basi hatokosea mwongozo. Yule anayemuomba mshauri nasaha basi kamwe hatojuta.

10 – Moja katika sifa za mwenye busara wakati wa matatizo ni yeye kumuomba ushauri mtu mwenye akili na mwenye kuwatakia wengine mema kisha baada ya hapo amtii. Anapaswa kutambua haki wakati wa mashauriano na wala asiminyane ndani ya batili. Badala yake anapaswa kuikubali haki pasi na kujali imetoka kwa nani. Asiyadharau maoni matukufu yenye kutoka kwa mtu duni. Lulu yenye hatari haichafuliwi na hatari adimu ya mzamiaji. Kisha baada ya hapo amwombe Allaah ushauri na atendee kazi maelekezo hayo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Hibbaan al-Bustiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Rawdhat-ul-´Uqalaa’ wa Nuzhat-ul-Fudhwalaa’, uk. 188-193
  • Imechapishwa: 17/08/2021