49. Mtu afunge kwa kufuata ratiba ya muda?

Swali 49: Je, mtu afuate ratiba ya muda inapokuja katika kuanza na kukata swawm katika Ramadhaan?

Jibu: Kwa hali yoyote anatakiwa kuzingatia kupambazuka na kuzama kwa jua. Hilo ndilo lililo salama zaidi. Ratiba ya muda inayoonesha kuamrisha swawm kabla ya kupambazuka ni jambo la usalama kwa uhakika.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaas-Swiyaam, uk. 68
  • Imechapishwa: 13/06/2017