49. Dalili ya ishirini na nne kutoka katika Sunnah juu ya mikono ya Allaah


51- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna mja yeyote muumini anayetoa swadaqah kutoka katika pato zuri – na wala Allaah hakubali isipokuwa kilicho kizuri – isipokuwa Allaah Anaiweka kwenye mkono wa Mwingi wa huruma na anailea kama anavyolea mmoja wenu kitekli chake ambapo tende inakuwa kama mlima mkubwa.”[1]

Hadiyth ni Swahiyh.

[1] Ahmad (2/431) na an-Nasaa’iy (4/418).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaat-ul-Yad li-Laah Swifatan min Swifwaatih, uk. 35
  • Imechapishwa: 11/07/2019