Swali 48: Je, inafaa siku ya ijumaa Khutbah ikasimamiwa na mtu na kuswalisha akasimamia mtu mwengine[1]?

Jibu: Kikosi cha wanazuoni wengi wameona kuwa Khatwiyb ambaye ametoa Khutbah sio sharti aswalishe pia kwa sababu ya kutokuwepo dalili juu ya hilo. Baadhi ya wanazuoni wengine wameenda kinyume na mtazamo huo na wakaona kuwa Khatwiyb wa ijumaa ni sharti pia aswalishe. Maoni ya sawa ni kwamba hapana vibaya kufanya hivo ikiwa haja imepelekea kufanya hivo.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (12/382).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Jumu´ah wal-Jamaa´ah, uk. 99
  • Imechapishwa: 05/12/2021