47. Ni bora kuswali Tarawiyh na imamu au nyumbani na familia?

Swali 47: Ni lipi lililo bora mtu aswali Tarawiyh pamoja na imamu au nyumbani pamoja na familia kwa kuwa wanafamilia hawajui kusoma Qur-aan?

Jibu: Hapana shaka kwamba kuswali nyumbani na kuswali na familia ndio bora zaidi. Inafaa vilevile akaswali na imamu kisha akarudi nyumbani kabla ya Witr kuswali na familia. Hakuna neno lau ataswali zaidi ya Rakaa´ kumi au kumi na tatu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuweka kiwango maalum cha Rakaa´. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswali Rakaa´ kumi na moja au kumi na tatu bila ya kuweka kiwango cha Rakaa´ maalum. Alimwambia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ´Abdullaah bin ´Amr (Radhiya Allaahu ´anhumaa):

“Nimepata khabari kwamba unaswali usiku mzima na wala hulali na unafunga mchana.” ´Abdullaah akasema: “Ndio, nafanya hivo.” Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia: “Usifanye hivo. Ukifanya hivo basi nafsi yako itachoka na macho yako yadhoofika. Nafsi yako kwako ina haki, familia yako kwako ina haki na mke wako kwako na haki. Kwa hiyo mpe kila mmoja haki yake.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuweka kiwango cha Rakaa´ maalum. Pindi mwanamke alipomjia ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) na kumueleza kuhusu swalah yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia:

“Fanyeni kile mnachoweza. Hakika Allaah hachoki mpaka nyinyi mchoke.”[2]

[1] al-Bukhaariy (1979) na Muslim (1159).

[2] Muslim (782).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaas-Swiyaam, uk. 65-67
  • Imechapishwa: 13/06/2017