46. Dalili ya tatu kutoka kwa Mtume kwamba Allaah yuko juu ya viumbe


44 – Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad ametukhabarisha: Abu Bakr at-Twuraythiythiy ametuhadithia: Abul-Qaasim at-Twabariy ametuhadithia: ´Iysaa bin ´Aliy ametuhadithia: ´Abdullaah bin Muhammad al-Baghawiy ametuhadithia: ´Aliy bin Muslim ametuhadithia: Sayyaar ametuhadithia: Ja´far bin Sulaymaan ametuhadithia: Thaabit ametuhadithia:

“Daawuud alikuwa akirefusha swalah, kisha akirukuu, halafu akinyanyua mikono yake kuielekeza mbinguni kisha akisema: “Ee Mfalme uliyoko juu ya mbingu! Kwako ndiko nimekielekeza kichwa changu! Watumwa wanawatazama wamola wao, Wewe ambaye unaishi juu ya mbingu.”[1]

[1] adh-Dhahabiy amesema:

”Mlolongo wa wapokezi wake uko salama.” (al-´Uluww, uk. 552)

al-Albaaniy amesema:

”Mlolongo wa wapokezi wake ni Swahiyh.” (Mukhtaswar-ul-´Uluww, uk. 669)

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 142
  • Imechapishwa: 21/06/2018