45. Kuhusu sanda ya Muhrim


40- Muhrim atakafiniwa ndani ya nguo zake ambazo amefia nazo. Hayo ni kutokana na maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu yule Muhrim ambaye alivunjwa shingo yake na ngamia:

“… na mumkafini katika nguo zake [ambazo amefanya Ihraam akiwa nazo]… “

Imekwishatangulia kwa ukamilifu wake katika kipengele cha 3 nambari. 8 ukurasa wa 12-13. Ziada hii ameipokea an-Nasaa´iy, vivyo hivyo at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam al-Kabiyr” (02/165) kupitia njia mbili kutoka kwa ´Amr bin Diynaar, kutoka kwa Ibn Jubayr, kutoka kwa Ibn ´Abbaas. Cheni ya wapokezi hii ni Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 82
  • Imechapishwa: 26/02/2020