44. Dalili juu ya vidole vya Allaah 3


44- Abu Hafsw ´Umar bin Ahmad bin ´Aliy ad-Dawriy ametuhadithia: Muhammad bin ´Uthmaan bin Karaamah ametuhadithia: ´Abdullaah bin Numayr ametuhadithia, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Yaziyd ar-Raqqaashiy, kutoka kwa Anas bin Maalik ambaye amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akikithirisha kusema: “Ee Allaah! Uthibitishe moyo wangu katika dini Yako.” Baadhi ya Maswahabah wake wakasema: “Unachelea juu yetu ilihali tumekuamini na tumekuwa na yakini juu ya yale uliyokuja nayo kwetu?” Akasema: Ndio. Kwani hakika nyoyo ziko kati ya vidole viwili katika vidole vya Mwingi wa huruma (´Azza wa Jall). Anazigeuza.” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaashiria kwa vidole vyake.”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 91-92
  • Imechapishwa: 01/04/2018