42. Hakuna chochote kinachomtia Allaah uzito


Hakumtii uzito kuzihifadhi mbingu wala ardhi. Anazihifadhi na kuzibeba kutokana na uwezo Wake:

إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ

“Hakika hayo kwa Allaah ni mepesi.”[1]

Yeye ndiye ambaye anazizuia mbingu na ardhi kutokana na uwezo Wake. Hakumkalifishi chochote. Kwake hakuna zito. Hakumchoshi kuvihifadhi viwili hivyo.

[1] 35:11

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 35
  • Imechapishwa: 27/07/2021