40. Wudhuu´ kwa anayetokwa na utoko baadhi ya nyakati


Swali 40: Akitawadha yule ambaye anatokwa na utoko huo baadhi ya nyakati na baada ya kumaliza kutawadha na kabla ya kuanza kuswali akatokwa na utoko kwa mara nyingine – ni kipi kinachomlazimu?

Jibu: Ikiwa unamtoka baadhi ya nyakati peke yake basi asubiri mpaka ufike wakati ambao utoko huo umekatika. Ama akiwa hana hali ya kupambanua pindi unakatika na pindi haukatiki, basi atatakiwa punde tu baada ya wakati kuingia na ataswali na hakuna neno juu yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 60 su-aal wa jawaab fiy Ahkaam-il-Haydhw, uk. 36
  • Imechapishwa: 13/08/2021