40. Ni ipi hukumu kutumia vidonge katika Ramadhaan ili kuzuia hedhi?

Swali 40:  Ni ipi hukumu ya kutumia vidonge vya kuzuia hedhi katika Ramadhaan tu kwa lengo la kufunga mwezi mzima?

Jibu: Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amewaruhusu wanawake kutofunga wakati wa hedhi na nifasi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Sijapata kuwaona wapungufu wa akili na dini kama nyie, mwanaume mwenye busara anaweza kupotoshwa na mmoja wenu.” Wakauliza: “Ni upi upungufu wa dini na akili yetu?” Akasema: “Kuhusu upungufu wa akili yake, Allaah amefanya ushahidi wa wanawake wawili ni sawa na ushahidi wa mwanaume mmoja. Ama upungufu wa dini yake, anapokuwa na hedhi hafungi na wala hawaswali.”[1]

Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amemruhusu mwanamke kutofunga kipindi yuko na hedhi na nifasi. Hahitajii kutumia vidonge ili kufunga mwezi mzima. Isitoshe ni kwamba vidonge hivi vinawaathiri wanawake ndio maana wanatakiwa kuviepuka.

[1] al-Bukhaariy (304) na Muslim (80).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaas-Swiyaam, uk. 58-59
  • Imechapishwa: 13/06/2017