40. Mume amuonyeshe mke tabia nzuri


Miongoni mwa haki za mke juu ya mume wake amuoneshe tabia njema. Muonekano wake mzuri kwake uwe wazi. Kuna wanaume ambao wana tabia zilizo nzuri kabisa wakati wanapokuwa kwenye masoko, na marafiki zao na watu wengine wote. Katika hali hii muonekano wao ni mzuri. Pale tu wanapoingia nyumbani wanakuwa wabaya. Hawaonyeshi muonekano wowote mzuri. Wanakuwa ni wenye khasira na matusi. Hawasemi kamwe kitu kizuri. Hawafanyi kamwe kitu kizuri. Huwezi kuwasikia kamwe wakisema neno zuri. Ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Waumini wenye imani kamilifu zaidi ni wale wenye tabia nzuri kabisa na wabora wenu ni wale ambao ni wabora kwa ahli zao.”[1]

Hamna kheri yoyote kwako ikiwa unawasaidia marafiki zako na kutangamana nao vizuri midhali si mwenye kheri kwa familia yako. Ikiwa wewe ni mwenye kheri kwa familia yako na kuongezea juu ya hilo ukawa ni mwenye kheri kwa watu wote; ninakubashiria uko katika kheri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mbora wenu ni yule ambaye ni mbora kwa familia yake na mimi ni mbora wenu kwa familia yangu.”[2]

[1] at-Tirmidhiy (1162) na Ahmad (2/250 na 2/472). Muungo ni wa at-Tirmidhiy ambaye amesema:

“Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”

Kwenye mnyororo kuna Muhammad bin ´Amr bin ´Alqamah ambaye ni mwaminifu lakini anakosea, jambo ambalo limetajwa kwenye ”at-Taqriyb” (6228). Hadiyth ni Swahiyh kwa njia zake mbali mbali na kwa mapokezi yanayoitolea ushahidi kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”as-Swahiyhah” (284).

[2] ad-Daarimiy (2/2260), at-Tirmidhiy (3895) na Ibn Hibbaan (9/4177). at-Tirmidhiy ameseema:

”Hadiyth ni geni na Swahiyh.”

Hadiyth ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”as-Swahiyhah” (285) na (1174).

 

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqq-uz-Zawjayn, uk. 57-58