40. al-Qummiy upotoshaji wa nane wa al-Baqarah


al-Qummiy amesema wakati alipokuwa anafasiri Aayah:

وَلَيْسَ الْبِرُّ بِأَن تَأْتُوا الْبُيُوتَ مِن ظُهُورِهَا وَلَـٰكِنَّ الْبِرَّ مَنِ اتَّقَىٰ ۗ وَأْتُوا الْبُيُوتَ مِنْ أَبْوَابِهَا

“Na si wema kuingia nyumba kwa nyuma yake; lakini wema ni kwa kumcha Allaah. Na ingieni nyumba kupitia milango yake [ya mbele].” (02:189)

“Aayah imeteremshwa kwa mnasaba wa Kiongozi wa waumini (Rahimahu Allaah) ambaye Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema juu yake:

“Mimi ndio mji wa elimu na ´Aliy ndio mlango wake.””[1]

Hapa al-Qummiy amekusanya mambo mawili mabaya sana:

1- Amepotosha Maneno ya Allaah kutoka mahala pake na kusema kwamba Aayah imeteremshwa kwa mnasaba wa ´Aliy.

2- Ametumia dalili kwa Hadiyth iliyozushwa ambayo inanasibishwa kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa uongo.

[1] Tafsiyr al-Qummiy (1/68).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 75
  • Imechapishwa: 19/03/2017