Swali 04: Inajuzu kwetu sisi wanaume kumuuguza mgonjwa mwanamke na khaswa ikiwa kuna wauguzi wanaume pekee?

Jibu: Ni lazima kwa hospitali zote ziwe na wauguzi wa wanaume na wauguzi wa wanawake. Hili ni jambo la wajibu. Kama ambavo kunapaswa kuwepo kwa madaktari wa wanaume na madaktari wa wanawake. Isipokuwa tu wakati wa dharurah kubwa kwa mfano maradhi hayajulikani na yeyote isipokuwa mwanaume tu. Katika hali hiyo hakuna neno akamtibu mwanamke kwa sababu ya dharurah. Kadhalika ikiwa ugonjwa wa mwanaume fulani haujulikani isipokuwa na mwanamke. Katika hali hiyo hakuna ubaya akamtibu. Vinginevyo lililo la wajibu wanaume wawe na madaktari wao na wanawake wawe na madaktari wao. Hili ndilo jambo la lazima. Vivyo hivyo wawepo wauguzi wa wanaume na wauguzi wa wanawake. Lengo ni kuzuia njia za fitina na faragha zilizoharamishwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Mariydhw, uk. 22-23
  • Imechapishwa: 03/05/2019