4. Mara ya kwanza kujitokeza kwa Suufiyyah

Kuhusiana na historia ambapo Suufiyyah walipoanza kujitokeza, tamko la “Suufiyyah” lilikuwa halijulikani katika zama za Maswahabah. Bali lilikuwa halijulikani hata katika karne tatu ambazo ni bora. Jina hili lilitangaa baada ya karne hizo tatu. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema kwamba kujitokeza mara ya kwanza kwa Suufiyyah ilikuwa al-Baswrah ´Iraaq. Huko kulikuwa baadhi ya watu waliopetuka mipaka katika ´ibaadah na kuipa nyongo dunia – jambo ambalo kamwe lilikuwa halijaonekana mahala kwengine[1].

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (06/11).

  • Mhusika: Shaykh Muhammad bin Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqiyqat-us-Suufiyyah
  • Imechapishwa: 23/12/2019