Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alizaliwa siku ya Jumatatu nyusiku mbili za mwisho Rabiy´ al-Awwal. Kumesemekana pia ya kwamba amezaliwa tarehe nane. Kumesemekana pia kuwa ni tarehe tisa. Kumesemekana vilevile tarehe kumi na mbili. az-Zubayr bin Bakkaar amesema:

“Alizaliwa Ramadhaan.”

Hata hivyo kauli hii haina nguvu. Ameinukuu as-Suhayliy katika kitabu chake “ar-Rawdhwah”.

Alizaliwa mwaka wa tembo, miaka khamsini baada ya tukio hilo. Maoni mengine yanasema kuwa alizaliwa miaka thamanini na tano baada ya tukio hilo. Maoni mengine yanasema pia kuwa alizaliwa miaka kumi baada yake. Imesemekana vilevile ya kwamba alizaliwa miaka thalathini baada ya mwaka wa tembo. Maoni mengine yanasema ni miaka arubaini baada yake.

Maoni sahihi ni kwamba alizaliwa mwaka wa tembo. Ibraahiym bin al-Mundhir al-Hizaamiy (mwalimu wa al-Bukhaariy), Khaliyfah bin Khayyaat na wengine wamesimulia maafikiano juu ya hilo.

Baba yake alikufa kabla ya kuzaliwa. Maoni mengine yanasema kuwa alikufa wakati alipokuwa na miezi kadhaa. Maoni mengine yanasema kuwa alikufa pindi alipokuwa na mwaka mmoja. Maoni mengine yanasema pia kuwa alikuwa na miaka miwili.

Kauli ya kwanza ndio yenye kujulikana.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Kathiyr ad-Dimashqiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fusuwl fiy Siyrat-ir-Rasuwl, uk. 15-16
  • Imechapishwa: 18/03/2017