39. Unasemaje kwa ambao wanaeneza mikanda na makala zinazowasema vibaya walinganizi Salafiyyuun?

Swali 39: Tumesikia kuwa kuna mkanda unaoenezwa kati ya safu za vijana na watu wasiojulikana. Malengo ilikuwa ni kuchafua sura ya mwanachuoni mmoja miongoni mwa wanachuoni wa Sunnah na wenye kutetea mfumo wa ki-Salafiy na wenye kuihami nchi hii iliyobarikiwa kutokana na Bid´ah zenye kupotosha. Akamsaidia – yaani mwanachuoni huyo – Shaykh Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy ambaye alikuwa ni raisi wa kitengo cha Sunnah katika chuo kikuu cha Kiislamu hapo kabla. Una maelekezo yoyote kuhusiana na maudhui hii?

Jibu: Hakika waliofanya hivi kueneza mkanda huu ni kutokana na chuki walionayo  kwa Ahl-us-Sunnah, walinganizi wa Da´wah ya as-Salafiyyah na wanachuoni wa Salafiyyah. Ambaye alifanya hivo Allaah atamalizana nae.

Hakika mtu ambaye anataka kumjeruhi Shaykh mliyemtaja, ambaye ni katika Ahl-us-Sunnah kwa njia ya kwamba anaeneza Sunnah na kupambana na Bid´ah, anachotaka ni kueneza Bid´ah na anataka Sunnah itokomee. Hii ni dalili ya chuki walionayo Hizbiyyuun juu ya Ahl-us-Sunnah na juu ya watetezi wa Sunnah.

Haijuzu kwa yoyote kueneza mkanda huu wala kuutawanya. Sisi hatusema kuwa kuna ambaye amekingwa na kukosea. Inatokea wakati mwingine mtu anaponyokwa na neno pasi na kukusudia ambapo adui analichukua na kulifurahia na kuleta madai haya na yale juu yake. Uliyosema yanafanana na haya. Mtu huyo – yaani huyo Shaykh aliyeponyokwa na neno – bado ni katika Ahl-us-Sunnah, watetezi wa Sunnah na Tawhiyd. Anayemchukia ni mwenye kuichukia Sunnah. Ambaye anawakimbiza [watu] naye anawakimbiza mbali na Sunnah. Tunamuomba Allaah awahukumu kwa hekima na apatilize kati yao mapatilizo ya haraka ili aweze kuwafedhehesha mbele ya viumbe.

Miongoni mwa usulubu wao mbaya ni kuwa wanakata sentesi au neno na wanayaacha [maneno ya] kabla na baada yake ili yaeleweke vibaya. Hakika wamefikia kilele katika vitimbi na njama.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fataawaa al-Jaliyyah
  • Imechapishwa: 23/07/2017