39- ´Abdullaah bin ´Abdil-Jabbaar ametuhadithia: Muhammad bin Ahmad bin Mahbuub ametuhadithia: Abuu ´Iysaa ametuhadithia: ´Abd bin Humayd ametuhadithia: Muhammad bin Bishr al-´Abdiy na Ya´laa bin ´Ubayd wametuhadithia, kutoka kwa Hajjaaj bin Diynaar, kutoka kwa Abuu Ghaalib (Hazawwur al-Qurashiy kutoka Baswrah, pia alikuwa akijulikana kama mwanafunzi wa Ba´halah), kutoka kwa Abuu Umaamah (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna watu waliopotea baada ya uongofu waliyokuwemo isipokuwa baada ya kuanza kuleta mijadala.”

Kisha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasoma Aayah ifuatayo:

مَا ضَرَبُوهُ لَكَ إِلَّا جَدَلًا ۚ بَلْ هُمْ قَوْمٌ خَصِمُونَ

”Hawakukupigia mfano huo isipokuwa tu kutaka kubisha. Bali wao ni watu makhasimu.” [1][2]

Abuu Iysaa amesema:

“Hadiyth hii ni Swahiyh Swahiyh[3].”

Mwisho!

[1] 43:58

[2] at-Tirmidhiy (3253) na Ibn Maajah (48). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (141).

[3] ´Allaamah ´Aliy Naaswir al-Faqiyhiy amesema:

“Mchapishaji wa kitabu amekariri neno mara mbili. Kuna uwezekano inatakiwa iwe nzuri na Swahiyh.” (al-Arba´uun fiy Dalaa’il-it-Tawhiyd, uk. 92)

  • Mhusika: Imaam Abu Ismaa´iyl ´Abdullaah bin Muhammad al-Answaariy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´uun fiy Dalaa-il-it-Tawhiyd, uk. 78
  • Imechapishwa: 15/02/2017