38. Kupiga chafya (kuchemua) na kupiga miayo


161- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah Anapenda chafya na Anachukia miayo. Mmoja wenu akipiga chafya na akasema “Alhamdu lillaah” basi ni haki kwa kila Muislamu aliyemsikia kusema:

يَرْحَمُكَ الله

“Allaah Akurahamu.”

Ama kuhusu miayo, inatoka kwa Shaytwaan. Pindi mmoja wenu anapopiga miayo ajizuie awezavyo. Wakati mmoja wenu anapopiga miayo Shaytwaan hucheka.”

162- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mmoja wenu anapopiga chafya aseme:

الْحَمْدُ لله

“Himdi zote ni Zake Allaah:”

Ndugu yake, au swahibu wake, aseme kumwambia:

يَرْحَمُكَ الله

“Allaah Akurahamu.”

Ndugu yake akimwambia “Allaah Akurahamu” aseme:

يَهْدِيكم الله وَيُصْلِحُ بَالَكُمْ

“Allaah Akuongoze na Akutengenezee mambo yako.”[1]

Katika upokezi mwingine:

الْحَمْدُ للهِ عَلى كُلِّ حَال

“Himdi zote ni Zake Allaah kwa hali yoyote.”

163- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mmoja wenu akipiga chafya na akamhimidi Allaah amtakie Rahmah[2]. Ikiwa hatomhimidi Allaah asimtakie Rahmah.”

[1] Hii ni dalili ya wazi inayoonesha kwamba ni wajibu kusema “Allaah Akurahamu” kumwambia kila mwenye kumsikia anasema “Himdi zote ni Zake Allaah”. Kauli inayojulikana kwamba ni wajibu kwa baadhi ya watu tu (Fardhw Kifaayah) inakosa dalili hapa. Inakwenda kinyume na Hadiyth iliyotangulia (namba. 158)

[2] Yaani kumuombea kwa kusema:

يَرْحَمُكَ الله

“Allaah Akurahamu.”

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 102-104
  • Imechapishwa: 21/03/2017