37. Anayetokwa na utoko kukaa na Wudhuu´ muda mrefu

Swali 37: Inasihi kwa mwanamke huyo anayetokwa na utoko[1] kuswali swalah ya Dhuhaa´ kwa wudhuu´ wa Fajr?

Jibu: Si sahihi kufanya hivo. Swalah ya Dhuhaa´ imepangiwa muda maalum. Ni lazima kutawadha kwa ajili yake baada ya kuingia wakati wake. Kwa sababu mwanamke huyo ni kama mwanamke mwenye kutokwa na damu ya ugonjwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemwamrisha mwanamke mwenye kutokwa na damu ya ugonjwa kutawadha kwa ajili ya kila swalah.

Wakati wa Dhuhr ni tokea pale kupinduka kwa jua mpaka wakati wa ´Aswr.

Wakati wa ´Aswr ni tokea pale unapomalizika wakati wa Dhuhr mpaka pale jua linapopiga manjano. Huu ni wakati wa dharurah mpaka kuzama kwa jua.

Wakati wa Maghrib ni tokea pale jua linapozama mpaka kupotea kwa ule msitari mwekundu.

Wakati wa ´Ishaa ni kuanzia pale unapopotea msitari mwekundu mpaka nusu ya usiku.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/36-wudhuu-kwa-mwanamke-anayetokwa-na-utoko-nyakati-zote/

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 60 su-aal wa jawaab fiy Ahkaam-il-Haydhw, uk. 35
  • Imechapishwa: 01/08/2021