37. Ameshindwa kuendelea kumfuata imamu katika ijumaa kwa sababu ya kukatika kwa umeme

Swali 37: Watu wameswali swalah ya ijumaa msikitini katika ghorofa ya chini. Wakati wa swalah umeme ukakatika na hivyo waswaliji wakawa hawamsikii imamu. Hivyo akatangulia mmoja katika maamuma na akawakamilishia swalah. Ni ipi hukumu ya swalah ya watu hawa kwa vile amewakamilishia swalah kwa njia ya ijumaa? Ni ipi hukumu endapo mbele asingetangulia yeyote mbele; je, kila mmoja katika wao angekamilisha swalah yake peke yake? Ikiwa inafaa kufanya hivo; je, aikamilishe kujengea juu ya kwamba ni Dhuhr au ijumaa kwa vile mwanzoni alimsikia Khatwiyb, akaanza naye swalah na akaswali pamoja naye Rak´ah moja[1]?

Jibu: Ikiwa hali halisi ni ile iliyotajwa na muulizaji basi swalah zao wote ni sahihi. Kwa sababu ambaye amewahi Rak´ah moja ya ijumaa basi ameiwahi swalah ya ijumaa. Hivo ndivo ilivyopokelewa Hadiyth Swahiyh kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Asingetangulia mbele yeyote na kila mmoja akaswali kivyake Rak´ah ya mwisho basi hilo lingetosheleza. Ni kama ambaye amekuja amechelewa Rak´ah moja atatakiwa kuswali pamoja na imamu kile alichokidiriki kisha alipe Rak´ah ya pili kivyake. Hayo ni kutokana na ueneaji wa maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule atakayewahi Rak´ah moja ya swalah basi ameiwahi swalah.”[2]

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (12/331-332).

[2] al-Bukhaariy (546) na Muslim (954).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Jumu´ah wal-Jamaa´ah, uk. 77
  • Imechapishwa: 04/12/2021