36. Mwenye busara na kuitafuta kwake dunia


1 – Allaah (´Azza wa Jall) amemfanya mwanadamu kuwa ni mwenye kuipupia dunia itayotokomea ili isije kuharibika. Kwani ndio makazi ya wema na mahali pa kuchumia kwa wale wenye kumcha Allaah, waumini na waja wema. Kama watu wasingeipupia ingetokomea na kuharibika na hivyo matokeo yake mtu asingepata kitu cha kumsaidia ili aweze kutekeleza faradhi za Allaah sembuse yale mambo yaliyopendekezwa yanayonufaisha huko Aakhirah.

2 – Ni jambo lenye kusemwa vibaya mtu kuipupia sana.

3 – Ibn-ul-Mubaarak amesema:

“Ukarimu wa kutojali kile kilichomo mikononi mwa watu ni mkubwa zaidi kuliko ukarimu wa kujitolea kuwapa watu wengine. Muruwa wa kukinaika ni mkubwa zaidi kuliko muruwa wa kujitolea kuwapa watu wengine.”

4 – Ibn Siyriyn amesema:

“Kusipokuwa yale unayotaka basi taka yale yanayokuwa.”

5 – Tajiri mkubwa wa watu ni yule asiyekuwa mateka wa pupa. Fakiri mkubwa  wa watu ni yule ambaye pupa inamwongoza. Pupa ni sababu ya kupotea kwa mambo kutoka mahali pake. Pupa ni yenye kuharamishwa kama ambavo woga ni wenye kuua. Endapo pupa isingelikuwa na sifa yoyote mbaya isipokuwa kuhesabiwa kurefu siku ya Qiyaamah juu ya yale yote ambayo mtu alikusanya basi ingelikuwa inatosha kwa aliye na busara kutopupia dunia hii kwa wingi.

6 – Upuapiaji haufanyi kuzidi katika riziki. Jambo dogo analoadhibiwa kwalo mpuapia kwa pupa yake ni kunyimwa kustareheka na yale ambayo tayari amekwishapata. Matokeo yake anachoka kutafuta kitu ambacho hana uhakika kama atakipata au hatokipata. Kama mpupiaji angeacha kupupia kwa wingi  na badala yake akamtegemea Muumbaji wa mbingu basi Mola (´Azza wa Jall) angempa yale ambayo hakuyapupia.

7 – Pupa ni alama ya ufakiri. Choyo inapelekea katika umasikini. Choyo ni chanjo ya pupa. Mori ni chanjo ya ujinga. Kuzuia swadaqah ni nduguye pupa. Kiburi ni pacha wa ujinga.

8 – Abu ´Abdir-Rahmaan al-´Utbiy amesimulia kwamba baba yake amesema:

“Wana wa israaiyl waligombana juu ya Qadar kwa miaka 500. Kisha wakamwendea mwanachuoni mmoja ahawakumu. Wakamwambia: “Tueleze kuhusu Qadar. Lakini fanya kwa ufupi na ubainishe ili mjinga akuelewe.” Ndipo akasema: “Ni kukoseshwa kwa aliye na busara na kushinda kwa ambaye ni mjinga.”

9 – Yule anayetii pupa basi kamwe hatopata utulivu na raha. Pupa inapelekea katika majanga.

10 – Ni lazima kwa mwenye busara kutopupia dunia hii hivyo akawa ni mwenye kusimangwa duniani na Akahirah. Malengo yake iwe kutekeleza faradhi za Allaah. Yule asiyekuwa na malengo juu ya makusudio yake basi atajidhuru mwenyewe na kujichosha mwili wake. Ambaye yuko namna hii ni mwenye pupa yenye kusemwa vizuri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Hibbaan al-Bustiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Rawdhat-ul-´Uqalaa’ wa Nuzhat-ul-Fudhwalaa’, uk. 129-130
  • Imechapishwa: 18/08/2021