Swali 34: Je, inafaa kuswali ijumaa kabla ya jua kupondoka[1]?

Jibu: Inafaa kuswali ijumaa kabla ya jua kukengeuka. Lakini bora ni baada ya jua kupinduka kwa ajili ya kutoka nje ya makinzano ya wanazuoni. Kwa sababu wanazuoni wengi wanaona kwamba ni lazima swalah ya ijumaa iwe baada ya jua kupondoka, maoni ambayo ndio ya jopo kubwa la wanazuoni. Baadhi ya wanazuoni wengine wakaona kuwa inafaa kabla ya jua kupondoka mida ya saa sita. Zipo Hadiyth na mapokezi Swahiyh yanayofahamisha juu ya hilo. Ni sahihi akiswali punde kidogo kabla ya jua kupondoka. Lakini anatakikana asifanye hivo isipokuwa baada ya jua kupondoka kwa ajili ya kuzifanyia kazi Hadiyth zote na kutoka nje ya tofauti za wanazuoni na pia kuwafanyia wepesi watu wapate kuhudhuria wote na vilevile swalah ipate kuwa katika wakati mmoja. Hili ndio bora na salama zaidi.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (12/391-392).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Jumu´ah wal-Jamaa´ah, uk. 73
  • Imechapishwa: 03/12/2021