Swali 33: Je, inafaa kuzungumza kipindi ambapo imamu amenyamaza kati ya Khutbah mbili katika swalah ya ijumaa? Je, inafaa kuashiria kidole cha shahaadah kwenye mdomo bila kuzungumza kwa ajili ya kumzindua mtu asizungumze wakati wa Khutbah[1]?

Jibu: Inafaa kuzungumza kipindi ambapo imamu amenyamaza kati ya Khutbah mbili haja ikipelekea kufanya hivo. Hapana neno kumwashiria anayeongea na huku imamu anatoa Khutbah kwamba anyamaze. Ni kama ambavo inafaa kuashiria ndani ya swalah haja ikipelekea kufanya hivo.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (12/337).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Jumu´ah wal-Jamaa´ah, uk. 72-73
  • Imechapishwa: 03/12/2021