33. Du´aa ya kuingia kwenye kijiji au mji


141- Suhayb (Radhiya Allaahu ´anhu) ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuona kijiji ambacho alitaka kukiingia isipokuwa alisema wakati alipokiona:

اللهُمَّ رَبَّ السَّمواتِ السَّبْعِ وَمَا أَظْلَلْنَ وَرَبَّ الأَرْضِينَ السَّبْعِ وَمَا أَقْلَلْنَ وَرَبَّ الشَّيَاطِينِ وَمَا أَضْللنَ وَرَبَّ الرِّياح وَمَا ذَرَيْنَ أَسْأَلُكَ خيرَ هذِهِ الْقَرْيَةِ وَخَيْرَ أَهْلهَا وَخَيْرَ ما فيها وأَعوذُ بِكَ مِنْ شَرِّهَا وَشَرِّ أَهْلهَا وَشَرِّ مَا فيه

“Ee Allaah! Mola wa mbingu saba na kila ambacho zimekifunika. Mola wa ardhi saba na kila ambacho zimebeba. Mola wa Mashaytwaan na kila wanachokipoteza. Mola wa upepo na kila wanachokibeba. Ninakuomba kheri ya kijiji hichi, kheri ya watu wake na kheri ya vilivyomo ndani yake. Na ninajikinga Kwako na shari ya kijiji hichi, shari ya watu wake na shari iliyomo ndani yake.”

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 95
  • Imechapishwa: 21/03/2017