32. Ni yapi maoni yako juu ya kushiriki katika vituo vya majira ya joto?


Swali 32: Ni ipi hukumu ya kushiriki katika vituo vya wakati wa majira ya joto na kupoteza wakati huko? Ikiwa unaona kuwa kuna badala yake ni ipi?

Jibu: Sisemi kuwa vituo vya majira ya joto ni batili na kwamba vyote vina makosa. Kuna vituo ambavyo baadhi yake ni vya kheri na vingine vina shari. Kinachozingatiwa ni wale wenye kuvisimamia. Ikiwa wale wenye kuvisimamia ni wenye kufuata mfumo wa Salaf sahihi na njia ya salama na ´Aqiydah ya Salafiyyah sahihi, basi kushiri katika vituo hivyo inafaa bali imependekezwa kwa kuwa vina kheri. Ama endapo vituo hivi vitakuwa vinaeneshwa na watu wenye Bid´ah wapotevu na wenye kupoteza, Hizbiyyuun na watu wenye mfumo wa kimakosa, basi kushiriki katika vituo hivi vilivyo na sura kama hii haifai kwa kuwa vina shari na mwenye kushiriki humo atakuwa amejipelekea katika sa babu ya kujiangamiza ikiwa hatotubia kwa Allaah na kurejea Kwake. Hakika tumeona kwa watu hawa wenye mifumo kama hii mambo ya fedheha ambayo hayawezi kufanywa na mtu mwenye moyo uliyo na imani. Ikiwa wamefikia katika hali ya kusema kwamba kuna uhuru wa ´Aqiydah na kwamba kuna uhuru wa kuabudu na wanadai kuwa uyahudi na ukristo ni dini sahihi na wanaita katika umoja wa dini, kumebaki nini tena baada ya haya? Hivi kweli ni sahihi na inaingia akilini kwa yule ambaye anashuhudia ya kwamba hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad na ´Iysaa ni Mitume Wake kusema kuwa mkristo anayesema kuwa ´Iysaa ndiye Allaah, mwana wa Allaah au ana imani ya utatu kusema kwamba ni ndugu yake? Hapana. Au ni sahihi kwa muislamu kumwambia hivo myahudi ambaye anasema kuwa utume wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kwa waarabu peke yake? Allaah (Ta´ala) anasema kumwambia Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُمْ جَمِيعًا

“Sema [Ee Muhammad kuwaambia]: “Hakika mimi ni Mtume wa Allaah kwenu nyinyi nyote.”” (07:158)

Isitoshe ni jambo linalojulikana kuwa mayahudi ni ndugu wa ngedere na nguruwe. Hali zao zinajulikana. Hivi kweli inajuzu kwa muislamu kusema kuwa mtu kama huyu ni ndugu yake? Ninaapa kwa Allaah hii ndio dhuluma yenyewe pindi wanapojitokeza watu amabo wanadai kuwa wanalingania katika dini ya Allaah na wanaweka mikutano kwa ajili ya kuzifanya dini zote ziwe na umoja. Ametakasika Allaah! Hivi kweli itaaminika dini ya Kiislamu mwenye kusema na kulingania katika mambo kama haya? Si Allaah ndiye amesema:

إِنَّ الدِّينَ عِندَ اللَّـهِ الْإِسْلَامُ

“Hakika dini mbele ya Allaah ni Uislamu.”? (03:19)

وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ

“Na yeyote anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitokubaliwa kwake.”? (03:85)

  قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْا إِلَىٰ كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلَّا نَعْبُدَ إِلَّا اللَّـهَ وَلَا نُشْرِكَ بِهِ شَيْئًا وَلَا يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضًا أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ ۚ فَإِن تَوَلَّوْا فَقُولُوا اشْهَدُوا بِأَنَّا مُسْلِمُونَ

“Sema: “Enyi Ahl-ul-Kitaab! Njooni katika neno lililo sawa baina yetu na baina yenu: kwamba tusiabudu isipokuwa Allaah Pekee, na wala tusimshirikishe na chochote na wala tusiwafanye baadhi yetu kuwafanya wengine kuwa waungu badala ya Allaah.” Wakikengeuka basi semeni: “Shuhudieni kwamba sisi ni waislamu.”” (03:64)