Ikiwa kutoa mimba kunahitajia operesheni basi kuna hali tatu:

Ya kwanza: Mama na mtoto wote wanaishi. Hapa operesheni haijuzu isipokuwa kwa dharurah kwa mfano kuna uzito wa kuzaa kiasi cha kwamba kunahitajika operesheni. Hilo ni kwa sababu mwili ni amana kwa mja. Asiukhatarishe isipokuwa katika yaliyo na manufaa makubwa. Pengine akafikiria kuwa haitomdhuru na ikaja kumdhuru.

Ya pili: Mama na mtoto wote wamekufa. Hapa haijuzu kufanya operesheni kwa sababu hakuna faida ya kufanya hivo.

Ya tatu: Mama kuwa hai na mtoto amekufa. Hapa operesheni inajuzu ili kumtoa mtoto ikiwa hakukhofiwi madhara kwa mama. Kwa sababu lililo dhahiri – na Allaah ndiye mwenye kujua zaidi – ni kuwa kipomoko hakiwezi kutoka bila ya operesheni. Kuendelea kubaki tumboni kinazuia kushika mimba huko mbeleni na kunamdhuru. Huenda akawa mjane akiwa na ada yake.

Ya nne: Mama amekufa na mtoto yuhai. Ikiwa hakuna bahati yoyote ya mtoto kuishi haijuzu kufanya operesheni. Na ikiwa kuna bahati ya mtoto kuishi na sehemu katika mwili wake imetoka kwa nje kupitia kwa mama, lipasuliwe tumbo la mama ili kutoa mtoto aliyebaki. Na ikiwa hakukutoka kitu kupitia kwa mama, Hanaabilah wanasema lisipasuliwe tumbo la mama kwa sababu huko ni kumfanya akaonekana vibaya. Kauli sahihi ni kuwa inajuzu ikiwa hakuna njia nyingine ya kumtoa mtoto zaidi ya hiyo. Maoni haya yamechaguliwa na Ibn Hubayrah. Yanapatikana katika kitabu “al-Inswaaf”:

“Maoni haya ndio bora zaidi.”[1]

Hili linahusiana na khaswa hii leo ambapo upasuaji wa leo haufanyi kuumbuka. Litapasuliwa tumbo la mama kisha lishonwe tena. Isitoshe utukufu wa mtu aliye hai ni mkubwa kuliko utukufu wa ambaye kishakufa. Vilevile ni wajibu kuokoa uhai wa mtu ambaye ni haramu kumuua ikiwa ni pamoja na uhai wa mtoto tumboni mwa mama yake na Allaah ndiye anjua zaidi.

Angalizo: Katika hali ambayo inajuzu kutoa mimba kunahitajika kupatikane idhini ya mshirika mwenzio kama mume.

[1] al-Inswaaf (2/556).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Dimaa’ at-Twabiy´iyyah lin-Nisaa’ http://www.ibnothaimeen.com/all/books/article
  • Imechapishwa: 30/10/2016