31. Shubuha ya nne: “Washirikina wa zamani walikuwa wakiabudu miti na mawe tofauti na sisi” na majibu juu yake

Miongoni mwa shubuha zao ni kwamba wanasema kwamba washirikina wa mwanzo walikuwa wanaabudu miti, mawe na vitu visivyokuwa na uhai kidhahiri. Lakini sisi tunaomba au tunafanya Tawassul kwa waja wema na mawalii. Viumbe haw wana jaha mbele ya Allaah. Sisi tunawachukulia kama wakati kati baina yetu sisi na Allaah. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَابْتَغُوا إِلَيْهِ الْوَسِيلَةَ

”Enyi mlioamini!  Mcheni Allaah na tafuteni Kwake  ukuruba.” (al-Maaidah 05:35)

Sisi tumechukua ukuruba kwa kuwatumia watu hawa.

Tunawajibu kwa kuwaambia ukuruba (Wasiylah) kwa mujibu wa Qur-aan maana yake ni utiifu na ´ibaadah. Ukuruba ni yale mambo yanayomfikisha mtu kwa Allaah (´Azza wa Jall); kumtii,  kutekeleza maamrisho Yake na kuacha makatazo Yake. Ukuruba haina maana kwamba uweke baina yako wewe na Allaah mkati na kati. Hili halikufahamishwa na Qur-aan, Sunnah wala halikusema na mwanachuoni yeyote anayezingatiwa kwamba kuwa ukuruba ni kuweka wakati na kati. Bali ukuruba kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah ni kujikurubisha kwa Allaah kwa kumtii (Subhaanahu wa Ta´ala).

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَابْتَغُوا إِلَيْهِ الْوَسِيلَةَ

”Enyi mlioamini!  Mcheni Allaah na tafuteni Kwake  ukuruba.” (al-Maaidah 05:35)

bi maana kumkurubia Allaah na kumtii. Ama ambaye kafasiri kwamba ni kuweka mkati na kati, hii ni tafsiri batili na iliyozuliwa. Tafiri hii haikusemwa na yeyote katika maimamu wa tafsiri ya Qur-aan.

Kwa hali yoyote hizi ni shubuha batili na zisizokuwa na mashiko yoyote. Lakini ndio shubuha wanazotegemea.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 52-53
  • Imechapishwa: 02/08/2018