31. Du´aa wakati wa safari


133- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Yule anayetaka kusafiri aseme kuwaambia wale anaotaka kuwaacha:

أَسْتَوْدِعُكُمْ الله الذِي لا تَضيعُ وَدَائِعُهُ

”Ninawaacha chini ya ulinzi wa Allaah ulinzi ambao hauendi hivi hivi.”

134- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kile kinachoachwa chini ya ulinzi wa Allaah basi Allaah Hukihifadhi.”

135- Saalim amesema:

“Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) alikuwa akisema kumwambia mtu ambaye anataka kusafiri: “Njoo karibu yangu. Nitaagana na wewe kama jinsi Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyokuwa akiagana na sisi:

أَسْتَودعُ اللهَ دِينَكَ وأمانَتَكَ وَخَواتِيمَ أَعْمَالِكَ

”Ninaacha Dini yako, amana yako na kitendo chako cha mwisho katika ulinzi wa Allaah.”

136- Kuna mtu alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kusema:

“Ee Mtume wa Allaah! Ninataka kusafiri. Niwazadie kitu.” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Allaah Akuzawadie Taqwa.” Akasema: “Nipe zaidi.” Akasema: “Akusamehe dhambi zako.” Akasema: “Nipe zaidi.” Akasema: “Akusahilishie kheri popote ulipo.”

137- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu) ameeleza kwamba kuna mtu alisema:

“Ee Mtume wa Allaah! Mimi nataka kusafiri. Niusie.” Akasema: “Mche Allaah na sema “Allaahu Akbar” katika kila sehemu ya kupanda.” Wakati mtu yule alipotoka pale akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

اللَّهُمَّ اطْوِ لَهُ الْبُعْدَ وَهَوِّنْ عَلَيْهِ السَّفرَ

“Ee Allaah! Mfupishie umbali wake na msahilishie safari yake.”

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 91-93
  • Imechapishwa: 21/03/2017