31. Aina ya kwanza ya majina yaliyochukizwa


Imechukizwa kuwa na majina yafuatayo:

1- Majina yasiyokuwa yenye kuvutia katika maana yake, matamko yake na kimoja katika hayo. Majina kama hayo yanachochea mzaha, kuudhi na uchokozi seuze tusiseme kuwa yanaenda kinyume na uongofu wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mfano wa majina hayo ni Harb, Murrah, Khanjar, Fadhwiyh, Fahiytw, Hutwayhitw, Fadghuush… Mara nyingi majina hayo yanapatikana kwa mabedui. Mwenye kutazama kwenye orodha ya simu ataona maajabu katika pande fulani!

Majina mengine ya kuchukiza ni Huyaam na Suhaam. Yote mawili ni majina ya ngamia.

Imechukizwa vilevile kuitwa Rihaab na ´Aflaq kwa sababu yote mawili yana maana ilio mbaya.

Kadhalika Naadiyah ambayo maana yake ni “kuwa mbali na maji”.

  • Mhusika: ´Allaamah Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 25-26
  • Imechapishwa: 18/03/2017