30. Waandishi wajinga na wenye malengo mabaya wanaowakejeli watetezi imani sahihi juu ya Qur-aan

Kwa yule mwenye kushikamana na haki anakuwa siku zote juu ya ubainifu na ujuzi. Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah siku zote ni wenye kusema kuwa Qur-aan ni maneno ya Allaah, imeteremshwa na haikuumbwa. Kwake ndiko imeanza na Kwake ndiko itarudi. Ahl-us-Sunnah walipewa mtihani kutoka kwa Mu´tazilah kupitia mikono ya Ma´muun kuhusiana na masuala haya na Imaam Ahmad akaadhibiwa kwa sababu ya masuala haya. Ma´muun alikuwa anawalazimisha watu juu ya ´Aqiydah ya Mu´tazilah kuhusu Qur-aan na kwamba imeumbwa. Ahl-us-Sunnah wakapinga na kukataa. Aliyekuwa msitari wa mbele kabisa ni Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah). Alikataa kukubali na kunyenyekea maneno haya ya kimakosa. Allaah akamthibitisha juu ya imani na Allaah akawakosesha nusura Mu´tazilah na wale wenye kufuata mrengo wao. Hakuna walichopata isipokuwa fedheha  na kuangushwa.

Kwa masikitiko baadhi ya waandishi wanasema kuwa masuala ya kuumbwa kwa Qur-aan au kutokuumbwa ni mambo ambayo hayana faida yoyote na hayahitajii watu kugawanyika. Wanaona kuwa Imaam Ahmad alikosea wakati alipokataa na wengine wanaona kuwa ni mambo ya kisiasa. Hawakumuadhibu Imaam Ahmad kwa sababu ya msimamo wake kukataa kusema kuwa Qur-aan imeumbwa. Bali wanaona kwamba walimuadhibu kwa sababu waliogopa watu wasije kugeuka dhidi yao. Kwa hiyo ni mambo ya siasa. Hivi ndivo wanavosema hawa waandishi wajinga au watu wenye malengo mabaya. Wanasema kuwa masuala ya kusema kuhusu kuumbwa kwa Qur-aan hayastahiki haya yote. Hivi ndivo wanavosema. Kwa sababu ima ni wajinga hawajui khatari yake au ni wenye malengo fulani na Mu´tazilah ambao wanataka masuala haya yapite kwa watu. Wanasema kuwa hayastahiki mjadala wote huu. Haya yanapatikana hii leo katika magazeti yao na katika vitabu vyao.

Kwa kifupi ni kwamba mimi nimependa kuzindua haya ili asije yeyote kudanganyika na maandishi ya watu hawa. Wanasema kuwa masuala haya ni mepesi na hayahitajii Ruduud zote hizi. Bali ni masuala ya khatari sana. Tukikataa kuwa Qur-aan ni maneno ya Allaah tutakuwa tumebaki na kitu gani? Matokeo yake Shari´ah itabatilika. Kwa hiyo dalili na marejeo ya kwanza yatakuwa yameanguka kwa kubatilika Shari´ah. Hili ndio lengo la waanzilishi wa propaganda hii mbaya. Ingawa wengi katika wafuasi wa propaganda hii hawajui malengo yake. Lakini haya ndio makusudio. Inatosha kuwa maneno haya yametoka kwa mayahudi kupitia kwa al-Ja´d bin Dirhaam ambaye aliyapokea kutoka kwa mayahudi. Maneno yake:

“Naamini kuwa Qur-aan ni maneno ya Allaah. Yameteremshwa na hayakuumbwa.”

imeteremshwa, kama Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaanwanavosema Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Maneno yake:

“… hayakuumbwa.”

kama wanavosema Jahmiyyah na vifaranga vyao. Hii ndio ´Aqiydah ambayo ni lazima kwa muislamu kuiamini. Haifai kwake kusema kwamba haya ni masuala ya kishakilishakili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 50-51
  • Imechapishwa: 16/03/2021