30. Alikuwa halipi siku anazoacha kufunga kwa sababu ya hedhi

Swali 30: Mimi tangu nilipowajibikiwa na funga nilikuwa mwenye kufunga Ramadhaan. Lakini nilikuwa silipi masiku ninayoacha kufunga kwa sababu ya ada ya mwezi. Jengine ni kwamba sijui idadi ya masiku niliyokula. Anaomba mwongozo wa kile kinachomuwajibikia hivi sasa.

Jibu: Tunasikitishwa kutokea mfano wa mambo kama haya kati ya wanawake wa waumini. Kuacha kulipa funga ya zile siku zinazomuwajibikia ima kwa sababu ya ujinga au kupuuza, na yote mawili ni msiba. Kwa sababu ujinga dawa yake ni elimu na kuuliza. Kupuuza dawa yake ni kumcha Allaah (´Azza wa Jall), kumchunga, kuogopa adhabu Yake na kukimbilia yale yanayopelekea katika radhi Zake.

Ni lazima kwa mwanamke huyu kutubu kwa Allaah kwa yale aliyofanya na amwombe Allaah msamaha. Ajitahidi kuchunguza masiku aliyoacha kwa kiasi cha anavoweza kisha ayalipe. Dhimma yake itatakasika namna hii. Tunataraji kuwa Allaah atampokelea tawbah yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 60 su-aal wa jawaab fiy Ahkaam-il-Haydhw, uk. 27
  • Imechapishwa: 28/07/2021