30. al-´Ayyaashiy upotoshaji wa sita wa al-Baqarah

al-´Ayyaashiy amesema kuhusu Kauli ya Allaah (Ta´ala):

وَإِذْ قُلْنَا ادْخُلُوا هَـٰذِهِ الْقَرْيَةَ فَكُلُوا مِنْهَا حَيْثُ شِئْتُمْ رَغَدًا وَادْخُلُوا الْبَابَ سُجَّدًا وَقُولُوا حِطَّةٌ نَّغْفِرْ لَكُمْ خَطَايَاكُمْ ۚ وَسَنَزِيدُ الْمُحْسِنِينَ فَبَدَّلَ الَّذِينَ ظَلَمُوا قَوْلًا غَيْرَ الَّذِي قِيلَ لَهُمْ فَأَنزَلْنَا عَلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا رِجْزًا مِّنَ السَّمَاءِ بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ

“Na [kumbukeni] Tuliposema: “Ingieni mji huu [Quds] na kuleni humo maridhawa popote mpendapo na ingieni katika mlango [wake] huku mmeinama na semeni: “Tuondolee uzito wa madhambi yetu!” Tutakusameheeni makosa yenu na Tutawazidishia wafanyao wema.” Basi wale ambao wamedhulumu walibadilisha kauli [wakasema kauli] kinyume na ile waliyoambiwa, Tukateremsha juu ya waliodhulumu adhabu ya kufadhaika kutoka mbinguni kwa yale waliyokuwa wakifanya ya ufasiki.” (02:58-59)

“Sulaymaan al-Ja´fariy amesema: “Nilimsikia Abul-Hasan ar-Ridhwaa akisema kuhusu Kauli Yake Allaah:

وَقُولُوا حِطَّةٌ

“… na semeni: “Tuondolee uzito wa madhambi yetu!”

Akasema: “Abu Ja´far amesema: “Sisi ni mlango wa msamaha wenu.”

Zayd bin ash-Shahhaam ameeleza kuwa Abu Ja´far amesema:

“Jibriyl aliteremka na Aayah hii:

فَبَدَّلَ الَّذِينَ ظَلَمُوا

“Basi wale ambao wamedhulumu walibadilisha familia ya Muhammad… “

قَوْلًا غَيْرَ الَّذِي قِيلَ لَهُمْ فَأَنزَلْنَا عَلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا رِجْزًا مِّنَ السَّمَاءِ بِمَا كَانُوا يَفْسُقُونَ

“… kauli [wakasema kauli] kinyume na ile waliyoambiwa, Tukateremsha juu ya waliodhulumu kubadilisha familia ya Muhammad adhabu ya kufadhaika kutoka mbinguni kwa yale waliyokuwa wakifanya ya ufasiki.”[1]

Allaah Amemtakasa Abu ´Abdillaah na uongo huu. Aayah hizi mbili zinahusiana na wana wa Israaiyl jinsi walivoenda kinyume na Muusa. Wanabainisha jinsi walivyoadhibiwa kwa kwenda kwao kinyume na kubadilisha kwao kauli ya Allaah. Haina uhusiano wowote kabisa na familia ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni uongo mkubwa kabisa kwa Allaah kusema ya kwamba Aayah zinahusiana na wale waliowadhulumu kabla hata hawajazaliwa!

Miongoni mwa ukafiri na uongo ni yale aliyozidisha Raafidhwiy huyu kwenye Aayah hii:

“… na wakaidhulumu familia ya Muhammad.”

na kwamba Jibriyl ndio aliteremka nayo. Ni upotoshaji mchafu kabisa kuliko upotoshaji wa wana wa Israaiyl wa neno:

حِطَّةٌ

“Tuondolee uzito wa madhambi yetu!”

[1] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/45). Mhakiki ameeleza kwenye vitabu ”al-Bihaar” (7/26) na ”as-Swaafiy” (1/96).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 61-62
  • Imechapishwa: 19/03/2017