3. Hadiyth “Nyinyi hamshuhudii ya kwamba hapana… “

39- Jaabir bin Mutw´im amesema:

“Tulikuwa pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Juhfah ambapo akasema: “Nyinyi hamshuhudii ya kwamba hapana mungu wa kweli isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee hana mshirika, na kwamba mimi ni Mtume wa Allaah?” Tukasema: “Ndio.” Ndipo akasema: “Pateni bishara! Hakika hii Qur-aan ncha yake moja iko mikononi mwa Allaah na ncha yake nyingine iko mikononi mwenu. Shikamaneni nayo; hakika hamtopotea na wala hamtoangamia baada yake kamwe.”[1]

Ameipokea al-Bazzaar na at-Twabaraaniy katika ”al-Kabiyr” na ”as-Swaghiyr”.

[1] Swahiyh kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/453)
  • Imechapishwa: 26/04/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy