Lakini mawalii hawa si lazima Allaah apitishe karama kwa kila walii. Wako mawalii wengi wasiokuwa na makarama. Kwa sababu karama mara nyingi huja kwa ajili ya kuinusuru haki au kuizuia batili. Lengo sio kumthibitisha mtu kwa dhati yake. Kwa hiyo si lazima kila walii awe na makarama. Walii anaweza kuishi mpaka akafa pasi na kuwa na makarama kama ambavyo vilevile anaweza kuwa na makarama mengi. Wanachuoni wamesema kuhusu makarama haya kwamba kila karama yenye kutoka kwa walii basi hakika ni alama ya yule Mtume aliyemfuata. Sisemi kuwa ni ´miujiza`. Bora zaidi ni kusema alama. Hivo ndivo ilivosema Qur-aan. Alama ni bora zaidi kuliko miujiza. Kwa sababu hiyo ni alama juu ya ukweli wa yale aliyokuja nayo Mtume huyu. Miujiza inaweza kuwa kupitia mikononi mwa mchawi au kupitia mikononi mwa mtu mwenye nguvu ambaye anafanya mambo yasiyowezwa na wengine. Qur-aan imeita kuwa ni ´miujiza` hivyo na sisi tunasema hivo. Hivo ndo sahihi.

Kutokana na tunavosikia wapo watu ambao hii leo wanajiita kuwa ni mawalii. Lakini mwenye kuzingatia hali zao ataona kuwa wako mbali na uwalii na kwamba hawastahiki hivo kabisa. Lakini wako na mashaytwaan wenye kuwasaidia juu ya yale wanayoyataka. Kwa ajili hiyo wanawadanganya wale watu rahisi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy-´Aqiydah wal-´Amal, uk. 42-43
  • Imechapishwa: 22/08/2019