29. Msafiri na mgonjwa ambaye imependekezwa kwake kula

Imependekeza kuacha kufunga mgonjwa ambaye maradhi yanamdhuru na msafiri ambaye inafaa kwake kufupisha swalah. Amesema (Ta´ala) kuwahusu:

فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

“… basi atimize idadi katika masiku mengine..”[1]

Bi maana wale na walipe idadi ya zile siku walizokula. Amesema (Ta´ala):

يُرِيدُ اللَّـهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ

“Allaah anakutakieni mepesi na wala hakutakieni mazito.”[2]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakupewa khiyari kati ya mambo mawili isipokuwa alichagua lile lepesi zaidi[3]. al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Si katika wema kufunga safarini.”[4]

 Akifunga msafiri au mgonjwa ambaye swawm inamtia uzito funga zao zitasihi licha ya kwamba imechukizwa.

Ni haramu kwa mwanamke mwenye hedhi na mwenye damu ya uzazi kufunga kipindi cha damu zao. Isitoshe haitosihi.

[1] 02:185

[2] 02:185

[3] al-Bukhaariy (3560) na Muslim (5999).

[4] al-Bukhaariy (1946) na Muslim (2607).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mulakhasw al-Fiqh (01/391)
  • Imechapishwa: 26/04/2021